Famasia yako. Dawa, pesa na timu, sehemu moja.
Mauzo, stoo, expiry za dawa, supplier, zamu na ripoti, vyote sehemu moja. Unajua kinachoendelea dukani kwako bila kubahatisha.
Kila mtu anaona kazi yake.
Mmiliki, mfamasia na timu, kila mmoja na ruhusa yake, rekodi moja.
- 14Expiry inakaribiaNdani ya siku 60
- 6Stoo imepunguaChini ya kiwango
- 2Zinasubiri idhiniAngalia sasa
Kiswahili kwanzaRahisi kufundisha timu
Inafanya kazi kwenye simuSimu, tablet na kompyuta
Kila hatua ina mwenyeweRekodi kamili za kazi
Backup na updatesVipo ndani ya kifurushi
Famasia nzima inaongea lugha moja.
Ukiuza dawa, Rafiki inasasisha stoo, pesa, historia ya mteja na ripoti ya mmiliki, yote kwa mara moja. Hakuna kuandika kitu kilekile sehemu tatu.
Stoo inayokwambia kila kitu
Unaona kila batch, iko wapi, zimebaki ngapi, expiry lini, nini kimeingia na nini kimetoka.
- Alert stoo ikipungua
- FEFO na expiry control
Kaunta ya haraka, salama
Tafuta dawa haraka, kagua usalama wa mteja, pokea malipo, toa risiti, foleni inaendelea kusonga.
Mmiliki anaona biashara
Mauzo, faida, matumizi, madeni ya supplier na hatari, vyote vimekusanywa tayari kwa maamuzi yako.
Kila kazi, ruhusa yake
Mmiliki, mfamasia, mhasibu na mhifadhi wa stoo hawaingiliani, lakini rekodi zinaungana.
Nunua kutokana na uhitaji halisi
Panga manunuzi kutokana na mauzo, stoo iliyopungua na dawa walizoulizia wateja ukawa huna.
Ushahidi, si kumbukumbu tu
Kila idhini na kila badiliko limeandikwa: nani, lini, tawi gani, kifaa gani.
Mmiliki anaongoza biashara. Mfamasia anaongoza dawa.
Rafiki haimpi kila mtu kila kitu. Inampa kila mtu anachohitaji kufanya kazi yake vizuri, na inalinda mambo yasiyo yake.
Biashara yako leo
Kutoka usajili hadi mauzo ya kwanza.
Rafiki inakuongoza hatua kwa hatua. Hauhitaji kuwa mtaalamu wa kompyuta.
- 01
Fungua akaunti
Weka jina lako, namba ya simu na password.
- 02
Lipia kifurushi
TZS 35,000 kwa mwezi, au lipia miezi 6 na mwaka kwa punguzo. Unalipa salama kwa simu au kadi.
- 03
Weka taarifa za duka
Weka tawi, leseni, mmiliki na mfamasia wako aliyesajiliwa.
- 04
Weka dawa, anza
Ingiza dawa kwa CSV au moja moja, kisha anza kuuza.
Kifurushi kimoja. Famasia nzima.
Hakuna kulipia kila kitu kivyake. Unapata kila unachohitaji kuendesha tawi lako na timu yako.
Kabla ya kuanzaAndaa leseni ya famasia, taarifa za mfamasia aliyesajiliwa, bei zako na stoo ya kuanzia.
- Mwezi 1TZS 35,000
- Miezi 6TZS 140,000unaokoa TZS 70,000
- Mwaka 1TZS 300,000unaokoa TZS 120,000
Kwa famasia inayotaka control bila usumbufu.
- ✓Tawi 1 la famasia
- ✓Hadi wafanyakazi 10
- ✓Hadi vifaa 5
- ✓Mauzo, stoo, expiry na dawa
- ✓Supplier, matumizi na ripoti
- ✓Backup, updates na msaada
- ✓Siku 7 za neema baada ya kuisha
Rafiki inakusaidia kuamua. Haichukui nafasi ya mtaalamu.
- 01
Mfamasia bado anaamuaKupanga madaraja ya dawa, dawa za cheti na maamuzi ya kitaalamu, hayo yanahitaji mfamasia aliyesajiliwa.
- 02
Taarifa sahihi ni muhimuRipoti zinakuwa sahihi kama mauzo, stoo, bei na matumizi vimeingizwa sawasawa.
- 03
TRA ni mfumo tofautiRafiki haitoi risiti ya TRA mpaka kuwe na muunganisho rasmi uliothibitishwa.
Je, Rafiki ni mfumo wa mauzo tu?+
Hapana. Mauzo ni sehemu moja tu. Rafiki pia inaendesha stoo, expiry, dawa, supplier, manunuzi, zamu, matumizi, ruhusa na ripoti za mmiliki.
Mmiliki na mfamasia wanaona kitu kilekile?+
Hapana. Mmiliki anaona upande wa biashara. Mfamasia anaona kaunta, dawa, wateja, stoo na zamu. Kila mtu na kazi yake, kila mtu anawajibika.
Naweza kutumia simu yangu?+
Ndiyo. Rafiki inafanya kazi kwenye simu, tablet na kompyuta kupitia browser, hakuna programu ya kupakua.
Kifurushi kikiisha inakuwaje?+
Unapata siku 7 za neema kulipia upya. Zikipita, akaunti inasimama mpaka malipo yathibitishwe. Rekodi zako hazifutwi.
Naweza kuingiza stoo kutoka Excel?+
Ndiyo. Save faili yako kama CSV, ipakie, kagua kila mstari, kisha uthibitishe ndipo dawa na stoo ziandikwe.
Famasia yako inastahili Rafiki.
Anza leo, ujue dawa zako ziko wapi, pesa iko wapi na timu inafanya nini.